Thursday, 13 August 2015

MSAFARA WA LOWASSA WAZUIWA KUSHIRIKI MAZISHI YA MZEE PETER KISUMO
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro leo limeuzuia msafara wa mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa  wakati akielekea katika kwenye mazishi ya kada na Mwasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mzee Peter Kisumo huko Usangi, wilayani Mwanga. Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Maroro, wilayani humo.

Msafara wa Lowassa ulianza kukutana na kadhia hiyo katika eneo la Boma  Ng’ombe  baada ya jeshi hilo kuumamisha msafara huo na kuwazuia katika msafara wake, wanachi wengine walioongozana na mgombea huyo.

Mazishi ya kada huyo yalitarajiwa kuongozwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete huku taarifa zilizoufikia mtandao huu zikisemaa Lowassa pamoja na msafara wake walighaili kwa usalama wao kushiriki mazishi hayo baada ya msafara wao kuzuiwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment