Monday, 24 August 2015

LOWASSA ATUMIA USAFIRI WA DALADALA KUSIKIA MATATIZO YA WANANCHI DAR ES SALAAM


Mgombea urais kupitia umoja wa Katiba ya Wananachi (UKAWA) amezua gumza hii leo baada ya kutumia usafiri wa daladala katika maeneo ya Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.

Inadaiwa kuwa Mgombea urais huyo aliamua kupanda daladala  katika root ya Gongo la Mboto Chanika ili kujionea kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo hayo hali iliyozua tafrani kwa wananchi kutaka kumuona kufuatia tukio hilo kuwa la kushitukiza.

Katika hatua nyingine vyama vnavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA vimeshindwa kuzindua kampeni zake jijini Dar  es salaam jumamosi iliyopita kufuatia kuzuiwa na serikali kuutumia uwanja wa Taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia alisema kuwa umoja huo unatafakari ni wapi wakafanyie zoezi la kuzindua kampeni hizo kwa madai kuwa wanataka sehemu yenye usalama na itakayobebaba watu wengi zaidi kwa kuwa maeneo mengi ya wazi yalishauzwa kwa watu binafsi.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment