Thursday, 20 August 2015

KAYA MASIKINI KILOLO ZAPATA MGAO WA ZAIDI YA MILIONI 212 TOKA TASAFHALMASHAURI ya wilaya ya Kilolo imepokeza zaidi ya Sh Milioni 212.8 kupitia TASAF awamu ya tatu; zitakazowezesha kaya masikini 6,464 kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu.

Kaya hizo kwa mujibu Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Kilolo, Venance Mwaikambo zimetambuliwa, kuhakikiwa na kuandikishwa katika vijiji 70 kati ya vijiji 95 vya halmashauri hiyo.

Mwaikambo alisema kwa ujumla wake, halmashauri ya Kilolo ina jumla ya kaya zaidi ya 31,000.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango alisema zoezi la ulipaji wa fedha hizo limeanza Agosti 19 na litakamilika Agosti 22 kwa vijiji vyote 70 vya awamu ya kwanza ya mpango huo.

Alisema zoezi la malipo linafanywa na kamati za usimamizi za vijiji kwa kushirikiana na wawezeshaji ngazi ya wilaya na kwamba kaya hizo zinapata kati ya Sh 20,000 na 70,000.


Taarifa hii itakujia kwa kina hivipunde

Reactions:

0 comments:

Post a Comment