Friday, 28 August 2015

DK MAGUFULI AWALIPUA WANAONUNUA MADARAKA


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk John Magufuli amewalipua  wanasiasa wanao nunua madaraka akidai kwamba  wanaotumia fedha kuingia madarakani na kununua madaraka ipo siku watawauza waliowanunua.

Magufuli amesema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbalizi uliopo mkoa mpya wa Songwe, katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye stendi ya Mbalizi na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuongoza watanzania na kutatua matatizo yao.

Akizungumzia uzoefu wake serikalini, amesema ametumikia nchi hii kwa miaka 20 serikalini akiwa Waziri na amekuwa mkweli na muwazi, ndiyo maana ameweza kuisimamia vizuri kila Wizara au jukumu alilopewa na wakubwa wake, akiwatumikia watanzania na sasa anaomba nafasi ya urais ili aweze kutekeleza vyema jukumu lake la kuwatumikia watanzania.


Katika safari yake ya urais amesema hakutumia fedha yoyote, hivyo hakuna mtanzania yeyote anayemdai fedha, ila anadaiwa utumishi uliotukuka wenye uaminifu, kujituma na kutetea maslahi ya watanzania

Reactions:

0 comments:

Post a Comment