Thursday, 6 August 2015

DAR YAVUKA LENGO UANDIKISHAJI BVR DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Jaji Damian Lubuva.

Wananchi takribani milioni 2,845,256  sawa na asilimia 101.2 wameandikishwa  katika daftari la kudumu la wapiga  kwa kutumia mfumo wa BVR zoezi lililomalizika tarehe 4,8,2015.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi  Mh. Jaji  Mst. Damian  Z. Lubuva amebainisha kuwa  uandikishaji wa Wapiga kura kwa mkoa wa Dar es salaam ulianza rasmi julai 22 na kufanyika kwa siku 10  na hatimaye kuongezwa siku nne, jumla  ya  wananchi waliojitokeza na kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ilikuwa kama ifuatavyo:

Kinondoni jumla wapiga kura waliojiandikisha ni 1,157,617 sawa na 105%, wilaya ya Temeke wameandikishwa  886,564 sawa na 98%  na  wilaya ya Ilala wapiga kura  886,564 sawa na asilimia 98.9.

Ameongeza kuwa lengo lilikuwa ni kuandikisha wapiga kura 2,810,423 ambapo zoezi limeweza kuandikisha  jumla ya wapiga kura 2,845,256 sawa na 101.2%
Sambamba na kukamilisha uandikisha kwa BVR tume imeendelea  na zoezi la utoaji fomu za urais hadi sasa vyama vya siasa vitano wagombea wao wamechukua fomu.

Vyama hivyo ni United People Democratic Party(UPDP),Tanzania Labour Party(TLP), Democratic Party (DP)  Chama cha Umma  (Chauma) pamoja na chama cha Mapinduzi (CCM).

Tume ya uchaguzi imevitaka vyama vya siasa kuharakisha mchakato wa kuwapata wagombea urais na kuwasilisha ratiba kwenye makao makuu ya Tume  hiyo ili wapangiwe ratiba ya kwenda kuchukua fomu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment