Thursday, 27 August 2015

BI SAMIA AAHIDI VIWANDA VYA KUCHAKATA MADINI ARUSHA

Mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitajenga viwanda vya kuchakata madini ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuongeza vipato vyao.

Aidha kimeahidi kufufua viwanda vilivyosimama kikiwemo cha ‘General Tyre’ kama moja ya mipango yake ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Hayo yamesemwa na  mgombea mwenza nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kilombero, Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wana CCM na wananchi wengine.

Licha ya kujenga viwanda Bi. Samia amesema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri utakaotoa fursa za uhakika kwa akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo.

Kuhusu rushwa amesema serikali ya CCM italishughulikia suala hilo kwa vitendo, ili kuhakikisha wananchi wanapata haki na maendeleo wanayoyahitaji

Reactions:

0 comments:

Post a Comment