Saturday, 7 February 2015

WATU SITA WAFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO KIPUNGUNI DAR ES SALAAM

Nyumba ambayo marehemu hao walikuwa wanaishi, inavyoonekana kwasasa baada ya kuungua kwa moto
Baadhi ya wanafamilia katika majonzi
WATU sita wanaosadikiwa kuwa ni wa familia moja wamekufa baada ya kuunguzwa na moto ulioteketeza nyumba yao iliyopo Kipunguni jijini Dar es Salaam.

Watu hao ni wa familia ya David Mpilla ambaye ni mzazi wa mwanahabari Conrad Mpilla wa Redio Kitulo FM ya mjini Makete ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC).

Taarifa za mwanzo ambazo hata hivyo bado hazijathibitishwa na jeshi la Polisi zinaonesha chanzo cha ajali hiyo ni itilafu ya umeme iliyotokea katika nyumba hiyo.

Klabu ya wanahabari mkoa wa Iringa inaungana na familia hiyo katika msiba huo huku ikiwataka wanafamilia kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Mungu ametoa, Mungu ametwa,

Roho za marehemu zilazwe mahali pema peponi, AMEN.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment