Monday, 2 February 2015

SOMA HAPA YALIYOMKUTA MTOTO WA WHITNEY HOUSTON


Mtoto wa mwimbaji maarufu ambaye kwa sasa ni marehemu Whitney Houston ambaye alizaa na rapa Bobby Brown, Bobbi Kristina Brown jana alikutwa nyumbani kwake ndani ya bafu akiwa hajitambui.

Kwa mujibu wa polisi wa Roswell  watu wa huduma ya kwanza walifanikiwa kurejesha uhai wake na sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu katika hospitali ya  North Fulton .

Kwa mujibu wa TMZ, polisi wa Roswell walifika nyumbani kwa binti huyo Riverbend Manor saa 4:25 asubuhi jana baada ya mume  wake Nick Gordon akiwa na rafiki yake kumkuta ndani ya bafu akiwa hajitambui na kuanza kumpa msaada wa kwanza kabla ya kuita 911.

Whitney alikutwa amekufa Februari 2012 akiwa katika  bafu la hoteli ya Beverly Hills . Taarifa ya rasmi ya kifo ilielezwa kuwa ni matumizi ya mihadarati iliyomfanya azame kwenye bafu na kufa kwa kunywa maji.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment