Thursday, 5 February 2015

MKUU WA WILAYA YA MUFINDI NA DED WA MTWARA MJINI WAINGIA KATIKA TUHUMA YA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA


WAKATI wowote kuanzia sasa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evalista Kalulu na watumishi wengine wanne wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wake wa halmashauri, Limbakisye Shimwela wanaweza kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya Sh Milioni 3, fedha za umma.
Kwasasa Limbakiyse Shimwela ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Taarifa za uhakika zilizothibitishwa na DC Kalalu kwa njia ya simu alipokuwa akiongea na mtandao huu mapema hii leo zinaonesha fedha hizo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wilaya hiyo.
“Ni kweli, mimi na wengine wanne tunatuhumiwa kutumia kiasi hicho cha fedha vibaya. Fedha hizo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo,” alisema.

Alisema wamepata tuhuma hiyo kwa kile kinachoelezwa kwamba zilitumika bila kufuata taratibu za zabuni.
Habari kamili kuhusiana na tuhuma hiyo utaletewa hivikaribuni, endelea kuwa nasi…..

Reactions:

0 comments:

Post a Comment