Wednesday, 4 February 2015

MAGAIDI WA ISLAMIC STATE WAMCHOMA MOTO AKIWA HAI RUBANI WA JORDAN

Jordanian Pilot Muath al-Kasasba


KUNDI la kigaidi la Islamic State la Iraki, limetoa video inayoonesha jana Jumanne Rubani, raia wa Jordan akichomwa moto akiwa hai ndani ya ngome (kijichumba) iliyotengenezwa kwa nondo katika tukio linaloelezwa kuwa ni la kikatili zaidi kufanywa kwa mateka wa kigeni nchini humo.

Video hiyo ya Dakika 22 iliyosambazwa kwenye mitandao ya kompyuta inaonesha picha za Luteni Maaz al-Kassasbeh, aliyekamatwa mateka Desemba mwaka jana,akiwa anaungua na moto.

Al-Kassasbeh anaelezwa kuwa ni rubani wa kwanza kukamatawa mateka akishiriki mashambulizi ya Marekani dhidi ya waasi wa kijeshi nchini Syria na Iraki.

Mfalme Abdullah II aliahirisha ziara yake ya Washington na kurudi nyumbani, Televisheni ya Taifa imesema, baada ya kuthibitishwa mauaji ya rubani huyo mwenye umri wa miaka 26 huku serikali na jesho la Jordan likiahidi kulipa kisasi.

Jordan imelipiza kisasi cha kwanza, kwa kuwanyonga Sajida al-Rishawi na Ziad al-Karbouly, raia wa Iraki wanaohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaida, msemaji wa serikali Mohammed al-Momani amesema.

Mauaji hayo yamefanyika katika gereza la Swaga kilomita 80 kusini mwa Jordan katika mji wa Amman.

Mapema asubuhi ya leo, magari mawili ya kubeba wagonjwa yalionekana yakiondoka kutoka katika gereza hilo yakiwa yamebeba miili ya magaidi hao chini ya ulinzi mkali.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment