Thursday, 5 February 2015

BARAKA KIZUGUTO AWA AFISA HABARI MPYA WA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Baraka Kizuguto kuwa Ofisa Habari kuanzia Februari 1 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Kizuguto anayechukua nafasi ya Boniface Wambura alikuwa Ofisa Habari wa klabu ya Young Africans, nafasi aliyoitumikia kwa miaka miwili.

Kizuguto ana Stashahada ya Juu ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo cha LEARN IT cha Dar es Salaam. Pia ana ujuzi wa kusanifu tovuti, ufundi wa kompyuta na uchambuzi wa mifumo ya kompyuta.

Mei mwaka jana, Kizuguto aliteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhudhuria mafunzo ya usajili na uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao (TMS) yaliyofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.

Uteuzi huo umefanywa baada ya Septemba mwaka jana, TFF, kumeteua aliyekuwa Ofisa habari wake, Boniface Wambura  kuwa Mkurugenzi wa mashindano.

Wambura alichaguliwa na kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo baada ya kuonyesha nidhamu na utendaji kazi mzuri alipokuwa mwanahabari wake kwa kipindi kirefu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment