Saturday, 7 February 2015

AMTWANGA KICHWA MUMEWE NA KUMSABABISHIA KIFO

Kamanda Mwaruanda
MWANAMKE mmoja Clemencia Nowa (50) anashikiliwa na polisi baada ya kumpiga  kichwa mume wake na kumsababishia umauti. wanandoa hao ni wakazi wa kijijini cha Miangalua  wilayani Sumbawanga koani Rukwa.  

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda  alimtaja mume aliyekufa kuwa ni Stephen Shauri (72) na kusema mkasa huo ulitokea  alfajiri ya  Februari 04, mwaka huu  nyumbani kwao.

Akisimulia mkasa huo , Mwaruanda  alieleza kuwa   mara kwa mara majirani walimsikia   akimshutumu mume kuisaliti ndoa yao  lakini mume amekuwa akikana kutokuwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa yao .

Inadaiwa  asubuhi hiyo Clemencia  alimkwida  mumewe  na kumtandika kichwa  cha nguvu kilichosababisha aanguke  na kufa papo hapo .

Kwamujibu wa Kamanda Mwaruanda  mtuhumiwa huyo  alikamatwa na majirani zake  ambao walimfikisha  katika Kituo cha Polisi   Laela   . 
Source:Mchangiaji Rukwa 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment