Thursday, 5 February 2015

ALIYEMUUA POLISI NAYE AUAWA

PC SWAI
WAKATI mpiganaji aliyeuawa akijaribu kumuokoa mtoto wa miezi minane katika eneo la Chang’ombe Juu PC Joseph Swai anaagwa mchana huu , blogu hii imeelezwa kuwa mtuhumiwa Tisi Malya ameuawa na wananchi wenye hasira.

Imeelezwa kuwa baada ya kufanya kitendo cha mauaji na kukimbia wananchi walijikusanya na kumsaka na walipompata walimuua.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, David Misime  akihojiwa asubuhi ya leo alisema kwamba wananchi walijichukulia sheria mkononi na kwamba Polisi walipofika eneo hilo walikuta wananchi wameshamuua.

Alisema pamoja na kwamba wananchi walikuwa na hasira ya kuuawa kwa askari kipenzi wao hawakustahili kumuua mtuhumiwa huyo, walipaswa kusubiri afikishwe mahakamani.


Hata hivyo alisema kwamba mtuhumiwa alishawahi kufungwa miaka minne akamaliza na pia alishawahi kutumikia kifungo kingine  na wananchi walikuwa wakimuogopa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment