Sunday, 11 January 2015

WARIOBA NA TUME YAKE KULIPWA ZAIDI YA MILIONI 640 KAMA KIINUA MGONGO


ILIYOKUWA Tume ya Mabadiliko ya Katiba na watumishi wake wote, italipwa kiinua mgongo cha zaidi ya Sh Milioni 640 kutokana na kazi ya kuandaa rasimu waliyofanya kwa miaka miwili.

Tume hiyo iliyokuwa na watumishi 32, ilifanya kazi ya kukusanya maoni na kuandika rasimu mbili za Katiba kwa miaka miwili, iliwasilisha ripoti yake kwenye Bunge Maalumu la Katiba mwezi Machi mwaka jana, ikiwa ni kutimiza kifungu cha 31 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa anafikiria kuwalipa wajumbe wa tume hiyo aina fulani ya kifuta jasho ambacho kiwango chake atakiamua yeye na kwa wakati mwafaka na kulingana na rasilimali za Serikali.

Habari zinasema kuwa wajumbe wa kamati hiyo wanalipwa Sh20 milioni kila mmoja, tofauti na habari zilizokuwa zimezagaa kuwa kila mjumbe angelipwa Sh200 milioni. 
chanzo;mwananchi.co.tz

Reactions:

0 comments:

Post a Comment