Thursday, 8 January 2015

WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI NA ROLI, WILAYANI MUFINDI


WATU wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Panuel Express mapema jana kugongana na lori katika kijiji cha Idetero wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi alisema inahusisha basi hilo lenye namba za usajili T 919 ACD na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 122 ALW, mali ya kampuni ya Trasisco ya mkoani Arusha

Roli hilo lililokuwa na tela namba T 203 ATS lilikuwa likielekea Makambako mkoani Njombe likitokea Mafinga, mkoani Iringa wakati basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea Dodoma.

Mungi alisema kabla ya ajali hiyo, dereva wa basi hilo alitaka kuyapita magari mawili yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Mmoja wa abiria wa basi hilo, Farida John alisema; “katika eneo hilo la ajali, sisi tulikuwa na shuka mlima na roli hilo lilikuwa linapandisha. Mbele yetu kuliwa na basin a roli bovu.”

Alisema jitihada za dereva huyo kulitoa basi hilo nje ya barabara ili kukwepa asikutane na roli hilo hazikuzaa matunda hali iliyosababisha ajali hiyo itokee.

Huku majina yao yakichelewa kupatikana, Kamanda Mungi alisema wakati watu wawili waliokuwepo katika basi hilo walifariki duniani papo hapo, wengine wawili waliokuwepo katika roli hilo nao walifariki dunia.


Alisema majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi ya mjini Mafinga na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa ya mjini Iringa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment