Thursday, 1 January 2015

WAKAZI WA TEMEKE WALIVYOLIPOKEA TAMASHA LA TUO8 JANUARY

Mtayarishaji nguli wa muziki wa kizazi kipya, Paul Mathyesse `P Funk' akichana mistari na msanii Fid Q katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar jana.
WASANII wa muziki wa kizazi kipya, jana walitoa burudani ya aina yake pamoja na elimu kwa vijana juu ya ushiriki wao katika masuala ya nchi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

Wakiongowa na  Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ pamoja na Niki wa Pili, wasanii aidi ya 10 waliwapagawisha mamia ya mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja hivyo kupata burudani na elimu hiyo.

Akizungumza kabla ya kuimba nyimbo zake kali,Mwana FA akitumia tamasha hilo lililopewa jina la ‘Tuonane Januari’, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuchagua viongozi wanaowataka.

“Vijana wenzangu.., tusisubili watu wengine watufanyie maamuzi.., ni sisi wenyewe tunatakiwa kuamua tunachokitaka, tushiriki kwenye masuala nyeti ya nhi.., kuna uchaguzi mkuu unakuja, vijana tuwe mstari wa mbele na tuchague viongozi tunaowataka,” alisema Mwana FA.

Mara baada ya kusema hayo, alianza kuimba nyimbo zake zinabamba kwa sasa ukiwemo, mfalme ambao uliwapagawaisha mashabiki wengi viwanjani hapo.
Mbali nma Mwana FA, pia Niki wa pili alipata mapoekzi makubwa viwanani hapo kwa nyimbo zake kali huku pia akisisitiza vijana kuchakua maamuzi sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Wanamuziki wengine waliokonga nyoyo za mashabiki wao ni pamoja na Shilole, Fid Q, Ditto, Linah, Navy and kenzo, Dogo Janja, Madee, Chegge, Temba, mwasiti na Stamina, ambao nyimbo zao ziliwafanya mashabiki waliojitokeza kuimba nao sambamba.

Tamasha hilo pia lilifanyika katika mikoa ya Njombe na Morogoro ambapo linalengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kuwa karibu na kushiriki matukio muhimu ya nchi hususani uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Oktoba mwaka huu.

PICHANI jUU:  Mkali wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA akitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya Mwembembe yanga, jijini Dar es Salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment