Saturday, 24 January 2015

LULU AMFUNGUKIA MSANII MARLOW ...AMPA KAULI NZITO.. HEBU TU SOMA HAPA ALICHOMWAMBIAMrembo na muigizaji wa filamu aliejijengea jina toka utotoni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambae kila mtu anajua kuwa huyu ni mshabiki mkubwa wa muziki na wanamuziki wa hapa bongo kwani mara kadhaa amekuwa akijitokeza na kuelezea hisia zake kuhusu nyimbo mbalimbali na wasanii mabilmabli kama Diamond, Ally kiba, Yamoto Band na wengine wengi.

Kwa mara nyingine tena leo kupitia mtandaoni ameonyesha hisia zake za kum-miss msanii  wa bongo Fleva ,Marlow ambae kwasasa ameoa na ana familia  ni moja kati ya wasanii waliotamba sana miaka mitatu minne iliyopita. Na hiki ndicho alicho kiandika;

"Kwani tulikukosea nini kaka!???mbona ukatuonjesha na kutuondolea burudani tena!???I believe ur talented tena sio kidogo, sio kwa kubana pua, sio kwa kusingiziwa pengine majukumu ya ki kazi au ya kifamilia yamebana. Lakini naamini u have something to offer the whole world....Rudi msaidiane kuendelea kupeleka mziki unapotakiwa kufika jmn...!
I'm a fan...a big fan unajua sana yani. Marlow Mkali"-Lulu alimaliza.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment