Sunday, 18 January 2015

CRISTIANO RONALDO AMWAGANA NA MPENZI WAKE IRINA SHAYKPENZI moto ile mbaya alilokuwa nalo staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa mrembo wake wa kirusi Irina Shayk limevunjika rasmi.

Ronaldo na Shayk wamedumu katika penzi lao kwa zaidi ya miaka mitano. Kuvunjika kwa penzi lao kulianza kubashiriwa miezi michache iliyopita baada ya Ronaldo kushindwa kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya mrembo huyo iliyopewa jina la Hercules.

Uvumi uliongezeka zaidi baada ya wawili hao kutoonekana pamoja wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2015.

Hitimisho la penzi lao lilijidhihiri moja kwa moja baada ya mrembo huyo, kama ilivyokuwa kawaida yake, kutomsindikiza mpenzi wake Ronaldo kwenye sherehe za utoaji wa tuzo za mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2014.


Katika tuzo hizo, Ronaldo aliibuka mchezaji bora wa dunia dhidi ya staa mwenzake, Llionel Messi wa Barcelona.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment