Tuesday, 30 December 2014

ZAWADI KWA WASHINDI WA MSOLLA CUP ZAWEKWA MEZANI

Profesa Msolla akikagua timu zinazoshiriki ligi hiyo
Hapa ilikuwa wakati akikabidhi vifaa vya timu hizo shiriki
Akikagua

Young Boys FC ya Tarafa ya Mazombe
Ng'ang'ange FC ya tarafa ya Kilolo
Mazombe FC ya tarafa ya Kilolo
Mtandika FC ya tarafa ya Mahenge
Ruaha Mbuyuni FC ya tarafa ya Mahange
Ng'ang'ange FC ya tarafa ya Kilolo
Ujumbe wa siasa kwa washiriki na wapenzi wa mchezo huo
MBUNGE wa Jimbo la Kilolo, Profesa Peter Msolla ameweka mezani vikombe vitatu na zaidi ya Sh Milioni 1.2 zitakazowaniwa na timu sita za soka katika hatua ya mwisho ya kutafuta mshindi wa Kombe la Msolla, wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Ligi hiyo inayopigwa kila mwaka kwa lengo la kuinua vipaji vya mchezo huo wilayani humo uzishirikisha timu za vijiji 106 vya tarafa tatu za wilaya hiyo, za Mahenge, Mazombe na Kilolo.

Akizindua hatua hiyo ya mwisho ya ligi hiyo inayozikutanisha timu mbili bingwa kwa kila tarafa, Profesa Msolla ambaye pia ni Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal alitoa pia msaada wa mipira na seti moja ya jezi kwa  timu hizo sita, vifaa vitakavyowasaidia kushiriki vyema michuano hiyo.

Mbali na kupewa vifaa hivyo, timu hizo zinapata huduma ya malazi na chakula katika kijiji cha ilula matalawe ambako michuano hiyo ya lala salama itapigwa hadi Januari 3, 2015 washindi watakapopatikana na kupewa zawadi zao.

Akizungumzia  zawadi kwa washindi, Profesa Msolla alisema “Mshindi wa kwanza atapata Sh 500,000 na kikombe, wa pili Sh 300,000 na kikombe, na wa  tatu Sh 200,000 na kikombe.”

Alisema tofauti na miaka iliyopita, mwaka huu mshindi wa nne hadi wa sita nao watajipatia zawadi ambazo ni Sh 100,000 kwa mshindi wa nne, Sh 75,000 kwa mshindi wa tano na wa sita atajinyakulia Sh 50,000.

Profesa Msolla alisema ameanzisha mashindano hayo akiwa na ndoto ya kuona wilaya ya Kilolo inakuwa moja kati ya wilaya zinazotoa wachezaji wa viwango vya juu nchini.

“Mpira ni ajira kubwa ndani na nje ya nchi; wapo wachezaji wanaolipwa mamilioni ya fedha na kujipatia utajiri mkubwa kwa kila dakika 90 za mchezo,” alisema.

Katibu Msaidizi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kilolo, Azayadi Mtati alisema hatua hiyo ya mwisho ya mashindano hayo itapigwa kwa siku sita.

Katika matokeo ya ufunguzi wa mashindano hayo yaliyopigwa juzi katika uwanja wa Ilula Matelewe, timu ya Young Boys toka tarafa ya Mazombe ilishinda kwa bao 3-0 dhidi ya timu ya Bomalang’ombe FC ya tarafa ya Kilolo.

Mechi nyingine ilihusisha timu ya Mazombe FC(Mazombe) iliyoshinda kwa bao 3-1 dhidi ya Ng’ang’ange FC (Kilolo) na Ruaha Stars (Mahenge iliyoibuka kwa ushindi wa bao 5-2 dhidi ya Mtandika (Mahenge).

Ligi hiyo inaendelea leo.....

Reactions:

0 comments:

Post a Comment