Sunday, 28 December 2014

GEORGE WEAH ASHINDA USENETA

George Weah speaking at a campaign rally in Liberia

ALIYEKUWA nyota wa soka duniani, George Weah ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa seneta nchini kwake Liberia katika uchaguzi ulioshirikisha wapiga kura wachache kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola.

Katika uchaguzi huo, Weah alipata asilimia 78 ya kura zote zilizopigwa kwa kiti cha kaunti ya Montserrado inayohusisha mji Mkuu wa Monrovia.

Alimshinda Robert Sirleaf ambaye ni mtoto wa kiume wa Rais wan chi hiyo, Ellen Johnson Sirleaf aliyepata asilimia 11 ya kura hizo.

Wengine walioshinda katika uchaguzi huo wa senata ni pamoja na Jewel Taylor, aliyekuwa mke wa aliyekuwa Rais wan chi hiyo anayetumikia kifungo gerezani na aliyekuwa kiongozi wa waasi Prince Johnson.


Weaha ambaye ni mwafrika pekee kutwa taji la mwanasoka bora wa dunia mwaka 1995, aligombea urais mwaka 2005 na kuangushwa na Bi Johnson Sirleaf katika uchaguzi wa marudio baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza ambao hata hivyo hakumpa asilimia zilizokuwa zinatakiwa ili atangazwe mshindi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment