Sunday, 28 December 2014

ALIYEJARIBU KUMUUA PAPA JOHN PAUL ATUA VATICAN NA KUTEMBELEA KABURI LA PAPA HUYO

Man Who Tried to Kill Pope John Paul II Puts Roses on His Tomb

YULE jamaa aliyetaka kumuua Papa John Paul 11 miaka 33 iliyopita amejitokeza Vatican Jumamosi na kuweka maua meupe aina ya Rose katika kaburi la papa huyo na kusema anataka kuonana na Papa Francis.

Mturuki, Mehmet Ali Agca, alimsababishia John Paul majeraha makubwa baada ya kurusha risasi nyingi katika jaribio lilishindwa kumuua papa huyo, St. Peter's Square, Mei 13, 1981.

Hata hivyo Papa huyo wa zamani alimsamehe Agca, na mwaka 1983 baada ya tukio hilo alikwenda kumtembelea katika gereza la Rome alikokuwa akitumikia kifungo cha maisha.

Mwaka 2000 Agca, 56, alirudishwa nchini kwake Uturuki aambako pia alishitakiwa kwa makosa mbalimbali likiwemo la kumuua mwandishi wa habari kabla ya kuachiwa huru mwaka 2010.

Shambulio dhidi ya Papa John Paul, aliyefariki mwaka 2005, limeendelea kuacha wingu zito ambalo maswali yake hayajibiki mpaka sasa.

Kikosi maalumu cha upelelezi cha nchini Italia kiliwahi kusema mwaka 2006 kwamba “bila shaka yoyote” shambulio hilo lilipangwa na viongozi wa zamani wa Soviet.

Kuhusu ombi lake la kukutana na Papa Francis, msemaji wa Vatican, Paroko Federico Lombardi alisema: "Ameweka maua juu ya kaburi la John Paul, tunadhani hiyo inatosha.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment