Sunday, 9 November 2014

WIVU WA KIMAPENZI WASABABISHA MKE AMCHARANGE MUMUWE MKONO


RPC Fraiser Kashai
Polisi mkoani Tanga inamshikilia Gladness Daniel (18) mkazi wa Kijiji cha Kwekivu kata ya Kibirashi wilayani Kilindi mkoani Tanga kwa tuhuma za kumkata mkono mume wake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Akizungumza katika kikao cha hali ya uhalifu mkoani Tanga kilichowashirikisha maofisa usalama barabarani jana, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Fraisser Kashai, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 8 usiku wakati mume wa mke huyo akiwa amelala.

Alimtaja majeruhi huyo kuwa ni Sharif Suleiman(25) ambaye ni mfugaji alikatwa mkono wa kushoto kwa silaha aina ya shoka na usiku huohuo mtuhumiwa kudaiwa kutoroka kwenda kwa shangazi yake anayeishi kijiji cha Songe.

Alisema uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa wawili hao walikuwa katika misigano ya ndoa kwa muda mrefu na kila mmoja alikuwa akimtuhumu mwenzake kwa kukosa uaminifu.


Kamanda Kashai alisema majirani walisema kuwa wenza hao kila siku walikuwa wakipigana na kutuhumiana kwa kila mmoja kumwendea mwenzake kinyume.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment