Tuesday, 4 November 2014

VIJIJI VYAWATOZA WANAOFANYA NGONO NA WANAFUNZI SH 300,000


BAADHI ya vijiji, vimeelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kujitungia kiholela na kuzitumia sheria zake ndogo kabla hazijakubalika na kupitishwa kisheria na mamlaka zinazohusika.

Afisa Takukuru kutoka ofisi ya taasisi hiyo mkoani Iringa, Ismail Bukuku alisema moja ya sheria ndogo inayotumiwa na baadhi ya vijiji inahusu kuwatoza faini ya hadi Sh 300,000 wanaume wanaokamatwa wakijihusisha kimapenzi na wanafunzi hasa wale wa shule za msingi.

Akiwasilisha mada ya rushwa katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Iringa kilichofanyika hivikaribuni mjini Iringa, Bukuku alisema matumizi ya sheria kama hizo yanaangukia kwenye makosa ya rushwa

Reactions:

0 comments:

Post a Comment