Sunday, 9 November 2014

MHADHIRI WA UJERUMANI AFA AJALINI IRINGA


Mhadhiri wa kujitolea wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) Dorosea Lehmani (64) raia wa Ujerumani amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea juzi mkoani Iringa.

Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Mtandika Wilaya ya Kilolo mkoani hapa barabara kuu ya Iringa-Morogoro ikihusisha gari aina ya Land Cruiser, ilisababisha vifo vya watu wawili na majeruhi mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja Goliata Kitangusi (17) mkazi wa Mufindi aliyekuwa akiendesha baiskeli kuwa ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Akifafanua zaidi Kamanda Mungi alisema ajali hiyo ilitokea baada ya gari mali ya Chuo Kikuu cha Iringa kumgonga mwendesha baiskeli Kitangus (17) na kumsababishia kifo palepale.

Alisema baada ya tukio hilo gari lilipinduka na kusababisha kifo cha raia huyo wa kigeni na kujeruhi wengine, mmoja amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Mungi alifafanua kuwa tukio hilo lilitokea saa 10.45 jioni na kuongeza kuwa gari lililohusika na ajali hiyo lilikuwa likiendeshwa na Daniel Lutengo Mkazi wa Iringa na ni mali ya Chuo Kikuu cha Iringa.

Alisema mwili wa Mjerumani huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ukisubiri taratibu za wahusika wa msiba 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment