Saturday, 1 November 2014

GUNIA MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA AINA YA MIRUNGI ZAKAMATWA MJINI IRINGA


GARI namba IT 113118 EPW lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Zambia limekamwata mkoani Iringa juzi likiwa na gunia mbili za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Dawa hizo zinazotambuliwa kwa majina mbalimbali mkoani hapa likiwemo jina la gut au gomba zilikamatwa katik gari hilo lililokuwa pia limepakia wahamiaji haramu watano toka Ethiopia.

Jeshi la polisi Mkoani Iringa linawashikilia watu saba katika matukio matatu tofauti likiwepo la watu watano ambao ni  raia wa kigeni kushikiliwa kwa tuhuma ya kuingia nchi bila ya kibali maalum.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, ACP Ramadhani Mungi amesema gari hilo lilikamatwa na askari wa usalama barabarani katika eneo la Checkpoint-Igumbilo, mjini Iringa.

Dereva wa gari hilo, Agrey Kapinga (29) na wahamiaji haramu hao, Tagae Namore (23), Sandeka Barisa (30), Tamisga Dekero(20), Morgosi Mushika (23) na Takiu Taspapu (19) wanashikiliwa na Polisi.

Wakati huo huo, Kamanda Mungi amesema askari polisi wakiwa doria katika maeneo ya Ugele, mjini Iringa walimkama Taitas Kitindi (54) akiwa na silaha 2 aina ya gobole, ganda lake la risasi pamoja na sare moja ya kampuni za ulinzi.

Baada ya mahojiano na uchunguzi wa jeshi hilo, imebainika kwamba Kitindi anamiliki silaha hizo kinyume cha sheria.


Kamanda Mungi amewaomba wakazi wa mkoa wa Iringa kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za uhalifu kwa wakati ili zisileta madhara kwao na majirani zao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment