Friday, 7 November 2014

BAADA YA DK ISHENGOMA KUTEMWA, WAKUU WA WILAYA ZA MKOA WA IRINGA NA NJOMBE MATUMBO JOTO

Kutoka kulia, Dk Leticiwa Warioba (wa pili kulia), Evarista Kalalu anayefuata, Gerald Guninita, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu na aliyekuwa RC wa Iringa Dk Christine Ishengoma
Sarah Dumba (kushoto), DC wa Ileje, Rose Sitaki (katikati) na Estalina Kilasi wa Wanging'ombe
BAADA ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma kutemwa katika mabadiliko madogo ya nafasi hizo yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 5, mwaka huu, taarifa za uhakika kutoka wilaya za mkoa wa Iringa na Njombe zinadai wakuu wa wilaya wako katika matumbo joto wakiwa hawajui nini hatma yao kama mabadiliko ya nafasi zao yatafanywa.

Taarifa kutoka baadhi ya wilaya hizo zinadai kwamba baadhi ya wakuu wa wilaya hawana matumaini ya kurudi katika nafasi zao kwa kile kinachodaiwa na walio jirani zao kwamba wameshindwa kutumiza malengo ya kazi za kiutendaji na kisiasa walizopewa.

“Hakuna uhakika kama wote waliopo watarudi, na kama watarudi basi baadhi yao wanatakiwa kutambua kwamba Mungu yupo pamoja nao,” kilisema chanzo kimojawapo.

Chanzo hicho kilisema; “hata kama wewe ungekuwa Rais, kwa jinsi ulivyofanya kazi na wakuu wa wilaya wa mikoa hii miwili unajua nani hastahili kurudi kwenye nafasi hiyo. Na hata kama atarudi basi jawabu ni moja tu, amalizie awamu ya Kikwete.”

Wakati mkoa wa Iringa unaunda na wilaya ya Iringa ambayo mkuu wake wa wilaya ni Dk Leticia Warioba, Kilolo inaongozwa na Gerald Guninita huku Mufindi ikiongozwa na Evarista Kalalu.

Kwa upande wa mkoa wa Njombe, wakati wilaya ya Njombe inaongozwa na Sarah Dumba, Makete inaongozwa na Josephine Matiro, Ludewa inaongozwa Juma Solomon Madaha na Wanging’ombe yupo Estalina Kilasi.

Taarifa inasema sio wote watakaorudi, mtandao huu na wewe tunaendelea kusubiri majibu yatakayotolewa wakati wowote kuanzia sasa.


Itaendelea……………………….

Reactions:

0 comments:

Post a Comment