Thursday, 6 November 2014

BAADA YA DK CHRISTINE ISHENGOMA KUTEMWA, WANAHABARI IRINGA WATARAJIE NINI KWA RC MPYA?


Dk Christine Ishengoma
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma ni mmoja kati ya wakuu wa mikoa watatu waliotemwa katika mabadiliko madogo ya nafasi hizo yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 5, mwaka huu.

Mbali na Dk Ishengoma wengine waliotemwa huku wakiahidiwa kupewa kazi zingine ni pamoja Kanali Fabian Masawe aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Tangu awasili mkoani Iringa mwaka 2010, Dk Ishengoma amefanya mengi; yaliyowapendeza na kuwaudhi baadhi ya watu wakiwemo wanahabari.

Mtandao huu unaendelea kupitia kumbukumbu mbalimbali za kiutendaji baina yake na wanahabari wa mkoa wa Iringa na itakuletea taarifa hiyo hivikaribuni.

Sambamba na taarifa hiyo, mtandao huu utakuletea wasifu wa Mkuu wa Mkoa Mpya wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza na mahusiano yake na wanahabari.

Itaendelea...........................

Reactions:

1 comments:

  1. Kitendo cha kudharau na kutojali mchango wa wanahabari katika jamii ni doa ambalo kamwe halitofutika.Daima tutamkumbuka kwa mema mengine kwani sisi pia tunaitumikia jamii hiyohiyo.

    ReplyDelete