Saturday, 1 November 2014

ASKOFU MAARUFU TZ GEOR DAVIE AVUNJA NDOA YA SEKRETARI WAKEAskofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya Upako, George David ‘Geor Davie’ yenye makao makuu yake jijini Arusha ndiye aliyetajwa na mahakama hiyo kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ya Pamella ambaye alikuwa ni sekretari wa kiongozi huyo wa dini baada ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ukionesha mapenzi kunaswa kwenye simu ya mwanamke huyo ukitokea kwa Geor Davie.
KIMENUKA! Ndoa iliyodumu kwa miaka 15 kati ya Wiston Lotta (52) na Pamella Geofrey (40) imevunjwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kufuatia ushahidi mzito uliotolewa mahakamani hapo kumridhisha Hakimu Hawa Mghuruta.


Askofu Geor Davie akiwa na wasaidizi wake. Ushahidi uliotolewa na mwanaume ulidai kuwa mgogoro wa ndoa yake ulitokana na mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Askofu Geor Davie.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment