Friday, 7 November 2014

12 WAFA KATIKA AJALI YA BASI NA TRENI


Watu kumi na watatu wamefariki katika ajali iliyotokea huko Kibereke, Ifakara mkoani Morogoro, kati ya basi la abiria la Al Jabir lenye namba za usajili T725 ATD lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Ifakara na treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akizungumza kwa njia ya simu, Hassan Masala amesema: "Chanzo cha ajali ni basi ambalo limeigonga treni, treni ambayo
ilikuwa inakatiza hapo kwa hivyo bahati mbaya ikawa imefika na
ikakatiza kwa hiyo ikagongwa kwa nyuma."

Masala amekaririwa akisema kuwa watu waliojeruhiwa ni 40 ambapo 14 wametibiwa na kuruhusiwa kurudi majumbani mwao huku 26 wakilazwa katika kituo cha afya cha Kibaoni na katika hospitali ya Mt. Francis, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa hospitalini hapo.

Naye Kamanda wa polisi Mkoani humo Leonald Paulo amenukuliwa akisema kuwa ajali hiyo ilitokea leo majira ya saa 9:15 alasiri.

Kamanda huyo alisema kati ya watu walioaga dunia, sita wanaume, wanne wanawake na wawili ni watoto wakike wenye umri kati ya miaka mitano na sita. Aliwataja marehemu watatu waliotambulika katika ajali hiyo kuwa ni Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62) wakazi wa Ichonde Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na polisi wanamtafuta waka wahesabu ni mmoja kati ya wakuu wa mikoa watatu Mbali na Dk Ishengoma wengine waliotemwa huku wakiahidiwa kupewa kazi zingine ni pamoja Kanali Fabian Masawe aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Tangu awasili mkoani Iringa mwaka 2010, Dk Ishengoma amefanya mengi; yaliyowapendeza na kuwaudhi baadhi ya watu wakiwemo wanahabari.

Mtandao huu unaendelea kupitia kumbukumbu mbalimbali za kiutendaji baina yake na wanahabari wa mkoa wa Iringa na itakuletea taarifa hiyo hivikaribuni.

 amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa na kuwahamisha wengine sita na watatu wengine kupangiwa kazi nyingine.

Wakuu wapya wa Mikoa hao ni pamoja na Bi. Halima Omari Dendego ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Bi. Amina Juma Masenza ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye nae amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Bwn. Magesa S. Mulongo ambaye atakua Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha,Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma,Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi,Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Wengine walioapishwa leo Ikulu ya Dar es salaam na Rasi Jakaya Kikwete ni pamoja na mhe Samwel William Shellukindo kuwa balozi na msaidi wa rais masuala ya diplomasia,Dkt Yohana Budeba kuwa katibu mkuu wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi,Injinia Mbogo Futakamba kuwa katibu mkuu wizara ya maji.


Mbali na hao pia wengine ni Dkt Donan Mmbando kuwa katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii,Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa balozi wa tanzania nchini Canada pia Mhe Charles Pallangyo kuwa katibu tawala wa mkoa wa geita na Bw Adoh Stephen Mapunda kuwa katibu tawala wa mkoa wa arusha.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment