Wednesday, 22 October 2014

SHERIA ITAKAYODHIBITI UHARIFU NA USAMBAZAJI WA PICHA ZA NGONO KWENYE SIMU YAJA

Januari Makamba
SERIKALI imeahidi kuja na sheria itakayoweka makatazo ya matumizi mabaya ya mitandao ya simu yanayohusisha usambazaji wa picha za ngono, wizi na taarifa zingine zinazochangia kubomoa maadili ya mtanzania.

Akizungumza na wanahabari wa mjini Iringa juzi, Naibu Waziri wa Masiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba alisema kuna uwezekano sheria hiyo mpya (cyber crime law) ikapelekwa bungeni Novemba mwaka huu.

Kwa kupitia sheria hiyo, Makamba alisema itakuwa ni marufuku kuweka picha za uchi, ngono na kutumia simu au mitandao ya kijamii kufanya uharifu au kusambaza kwa watu wengine taarifa zozote zinazoathiri maadili ya mtanzania.

“Mawasiliano ya simu ni kama kisu, kinatumika kwa mambo mazuri na mabaya, kujeruhi na kuua; na kama ilivyo kwa kisu, kuna tatizo kubwa kwenye mitandao, ikiwemo ya simu. Baadhi ya watu wanaitumia mitandao hiyo kwa mambo mengi yasiofaa,”


Alisema kwa kupitia sheria hiyo zitatengenezwa kanuni mpya za maudhui yanayoingizwa kwenye mitandao ili kudhibiti kila kitu kinachoingizwa kwenye simu au mitandao hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment