Friday, 17 October 2014

NYOTA 4 WA KIGENI KUFUNGA SERENGETI FIESTA 2014http://youthvillage.co.za/yvsabru/wp-content/uploads/2013/09/ti3.jpg
Clifford Joseph Harris
BAADA ya kuzunguka maelfu ya maili, Tamasha la Serengeti Fiesta 2014, litafunga ziara yake kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi, likihusisha wanamuziki wanne maarufu duniani.

Rapa wa kimataifa kutoka Marekani, Clifford Joseph Harris maarufu T.I pamoja na Waje kutoka Nigeria, Ash Hamman kutoka Dubai na nyota mwingine wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kenya, Victoria Kimani wanatarajiwa kutua leo nchini kwa ajili kuburudisha katika Tamasha la Serengeti Fiesta.

Wanne hao ndio wanamuziki wa kimataifa kutoka nje ya Tanzania watakaotumbuiza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 sambamba na wazawa akiwemo nyota wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz.’

T.I anatarajiwa kutua leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kwa ajili ya tamasha hilo ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka.

Shoo ya mwisho ya Serengeti Fiesta 2014 inatarajiwa kupambwa zaidi na wasanii wa nchini wanaotarajiwa kumsindikiza T.I ni Diamond Platnumz, Yamoto Band, TMK Wanaume Family, Weusi, Tip Top Connection, Ommy Dimpoz, Ali kiba, Mwana FA, Shaa, Vanessa Mdee, Recho, Linah, Barnaba, Mr. Blue, Young Killa, Ney wa Mitego na Stamina ambao wamepania kuthibitisha ile kaulimbiu ya mwaka huu kuwa ni Serengeti Fiesta “Ni Sheeedah.”

 Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager inayodhamini tamasha hilo, Rugambo Rodney alisema:

“Tulikuwa tukiisubiri kwa hamu siku hii na hakika kila kitu kipo sawa kama kilivyopangwa. Kazi yangu ni kuwahakikishia mashabiki wetu kwamba Kampuni ya Bia ya Serengeti pamoja na Primetime Promotions watafanya moja kati ya shoo bora kabisa kutokea katika mfululizo wa matamasha ya Serengeti Fiesta 2014 na hii inathibitishwa na idadi ya wasanii wa kimataifa na wazawa watakaotumbuiza.
 
Kabla ya onesho hilo la jioni, kulikuwa na shughuli nyingi za utangulizi likiwamo shindano la dansi la Fiesta ambapo majaji wa shindani hilo waliumiza kichwa katika kumpata mshindi  na hatimaye kundi la “Wazawa” lilijinyakulia zawadi nono ya Sh milioni tatu baada ya shoo nzuri iliyowavutia majaji.

Baadaye, lilifanyika shindano la kuimba la Super Nyota Divas ambapo Hellen George kutoka Dar  es Salaam atapambana na washindani wengine kutoka mikoani.

Serengeti Fiesta imeshafanya shoo katika mikoa 15 nchini mwaka huu, na iliwavutia maelfu ya mashabiki hasa katika miji ambayo ilipita kwa mara ya kwanza kama Kahama, Bukoba na Songea.
Source:Habarileo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment