Saturday, 18 October 2014

NIGERIA YAUFYATA KWA BOKO HARAMU, WAINGIA MAKUBALIANO

Add caption
NIGERIA imesema kwamba imefikia makubaliano ya kusitisha mapigano na wapiganaji wa Bokoharam na kundi hilo linalopigana kwa jina la dini  inasadikiwa limekubali kuwarejesha mabinti wote iliowateka.

Mkuu wa Unadhimu jeshi la Nigeria Alex Badeh, ndiye aliyetangaza makubaliano hayo ya amani lakini kundi la Boko haram lenyewe haliasema kitu.

Boko haram wamekuwa wakipigana na serikali ya Nigeria kutoka mwaka 2009 na watu zaidi ya 2000 wameshauawa.

Miezi sita Kundi hilo liliifanya dunia kuzizima baada ya kuwatekanyara mabinti wa shule 200 kwa mkupuo.


Mabinti hao walitekwa kaskazini mashariki mwa mji wa Chibok  uliopo katika jimbo la Borno.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment