Tuesday, 21 October 2014

MZEE WA MIAKA 74 AJITOKEZA NA KUDAI ANA DAWA YA KUTIBU UGONJWA WA EBOLA

Yahaya Chawe (74)

WAKATI dunia ikiwa katika hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola, Mzee Yahaya Chawe, mwenye miaka 74, ameibuka na kudai kwamba anayo dawa asilia inayoweza kutibu ugonjwa huo.

Katika mazungumzo yake na mtandao huu wa BONGO LEAKS hii leo, Chawe amesema; “dawa hiyo ya miti shamba inaweza pia kutibu kansa, vidonda na upele usiopona.”

Alipoulizwa dawa hiyo inatokana na aina gani ya mti shamba, Mzee Chawe anayeishi katika kijiji cha Mseke, nje kidogo ya manispaa ya Iringa, barabara ya Iringa Mbeya, alisema hawezi kutaja hata siku moja kwa kuwa atakuwa anauza ujuzi wake bure.

Hata hivyo aliitetea dawa hiyo akisema imepata mafanikio makubwa kwa wagonjwa wa kansa na wenye matatizo ya vidonda visvyopona.

Mnamo mwezi wa Machi 2014,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi ulioanzia Guinea na kusambaa katika nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Hadi tarehe 31 Julai, 2014 idadi ya wagonjwa ilikuwa 1323 na vifo 729.

Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi.

Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa:-
·                     kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa
·                     kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu.
·                     kugusa wanyama walioambukizwa, Mizoga na wazima

Reactions:

0 comments:

Post a Comment