Tuesday, 21 October 2014

MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS AFUNGWA MIAKA MITANO JELA

Oscar Pistorius
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka 5 baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa adhabu hiyo imetolewa baada ya mwanariadha huyo kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo majira ya saa mbili asubuhi, Jaji Thokozile Masipa,amesema adhabu hiyo ni  changamoto kwa mwanariadha huyo na kuongeza kuwa mahakama imelazimika kutoa hukumu hiyo kwani imejiridhisha na kwamba maamuzi hayo yataleta usawa wa pande zote kwenye kesi hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment