Thursday, 30 October 2014

MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA APPLE ATANGAZA YEYE NI SHOGA

Tim Cook
AFISA Mtendaji Mkuu (CEO) wa Apple Tim Cook amevunja ukimya baada yah ii leo (Alhamis) kutangaza kwamba yeye ni shoga na anajisikia burudani kuwa katika hali hiyo.

“Naomba niweka wazi: Najisikia furaha kuwa shoga, na kwa kuwa shoga naona hiyo ni moja kati ya zawadi kubwa nilizopewa na Mwenyezi Mungu,” alinukuliwa na Bloomberg Businessweek.

Katika chapisho hilo, Cook amesema alijitahidi kwa kadri alivyoweza “kuweka usiri.” Lakini akasema usiri huo ulimzuia kufanya kazi kwa faida ya wengine.

“Sijioni kama ni mwanaharakati, lakini natambua ni kwa kiasi gani nimefaidika kwa kupitia wengine waliojitoa muhanga,” alisema.

“Kwahiyo kwa kusikia kwamba Afisa Mtendaji Mkuu wa Apple ni shoga itasaidia kuwatoa wengine hadharani au kuongeza faraja kwa yoyote anayejisikia mpweke kwasababu hiyo, au kuwahamasisha watu kusisitiza juu ya usawa,” alisema.

Cook, aliyekulia Alabama, alisema amekuwa muwazi kuhusu hali yake hiyo, lakini hakuwahi kuidaili hadharani.  

“Wengi katika kampuni hii ya Apple wanajua kwamba mimi ni shoga, na hawajawahi kuonesha tofauti yoyote kwangu wanapofanya kazi na mimia,” alisema.

“Kwa kweli, imekuwa bahati kwangu kufanya kazi katika kampuni inayopenda ujuzi na ubunifu na inayojua kwamba itaendelea kukua ikiwakubali watu kwa tofauti zao. Sio kila mtu ana bahati.”

Kampuni ya Apple ni wazalishaji wa bidhaa za kielekroniki zenye umaarufu mkubwa duniani kote. Bidhaa hizo ni pamoja iPhone, iPod na iPad.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment