Thursday, 23 October 2014

KIMOTCO NA FROLIDA EXPRESS ZAVAANA USO KWA USO, ABIRIA ZAIDI YA 100 WANUSURIKA

Basi la Frolida baada ya ajali hiyo
Basi la Kimotco baada ya ajali hiyo
Baadhi ya abiria waliokuwemo katika mabasi hayo
Kimotco linavyoonekana kwa mbele baada ya ajali hiyo
ABIRIA zaidi ya 100 wamenusurika kufa katika ajali iliyotokea katika mlima Nyang’oro, barabara ya Iringa Dodoma.

Ajali hiyo iliyohusisha mabasi mawili, Kimotco lenye namba za usajili T449 CAL na Frolida lenye namba T571BDX ilitokea majira ya saa moja asubuhi ya leo.

Wakati Kimotco lilikuwa likielekea Arusha, basi la Frolida lilikuwa likitokea Mtera kwenda Iringa Mjini.

Mmoja wa watu aliyenusurika katika ajali hiyo ni Samsoni Kikoti wa mtandao huu wa BONGO LEAKS aliyekuwa katika basi la Kimotco akielekea mkoani Tabora.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa na Kikoti kwamba ni makini mdogo wa dereva wa basi la Frolida aliyafahamika kwa jina moja la utani la Dulayo kuendesha basi hilo kwa mwendo mkali kwenye kona kali za mlima huo.

Akiwa katika mwendo huo, dereva huyo alishindwa kumudu moja ya kona za mlima huo wakati akipishana na Kimotco na kusababisha ajali hiyo.


Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment