Tuesday, 28 October 2014

KILO 296 ZA BANGI NA LITA 479 ZA GONGO ZAKAMATWA JIJINI MBEYA


KILO 296 na gramu 678 za bangi zimekamatwa mkoani Mbeya katika kipindi cha kati ya Januari na Julai, mwaka huu.

Pamoja na bangi, jeshi la Polisi kwa msaada wa wasamalia wema liliweza kubaini na kuteketeza mashamba matatu ya bangi yenye ukubwa wa jumla ya ekari moja na robo.

Pamoja na bangi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahamed Msangi alisema lita 479 za gongo pamoja na mitambo 16 ya kutengenezea pombe hiyo vilikamatwa pia katika kipindi hicho.

Katika kipindi hicho, , watu 135 waliuawa katika matukio tofauti yaliyohusisha wananchi kujichukulia sheria mkononi, imani za kishirikina, wivu, ugoni, ugomvi majumbani, ugomvi vilabuni na ulipizaji kisasi.

Katika kipindi hicho, Msangi alisema jeshi la Polisi lilifanikiwa pia kukamata bunduki 19 , kati yake gobore zilikuwa 15, bastola mbili, riffle moja na SMG moja.
chanzo;kalulunga media

Reactions:

0 comments:

Post a Comment