Tuesday, 21 October 2014

JANUARI MAKAMBA AZUNGUMZIA DHAMIRA YAKE YA KUWANIA URAIS, AWAKANA WANAOMUHUSISHA NA LOWASSA

Januari Makamba
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba amesema hakuna mwanasiasa yoyote anayemuhofia kuwa kikwazo katika harakati zake za kuwania urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangaza nia hiyo April mwaka huu.

Wanaotajwa kuitaka nafasi hiyo kupitia chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho pia yeye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mizenho Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe na Waziri Ofisi ya Rais Uhusiano, Steven Wassira.

Wengine ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na wizara maalumu, Prof Mark Mwandosya, Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangalla, Naibu Waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba, Waziri wa Sheria na katiba Dk Rose Migoro na Waziri wa Maliasili na Utalii Razalo Nyalandu. 

Amewakana wote wanadai yuko nyuma ya Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa ambaye pia anatajwa kukitaka kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Na ameyapuuza madai ya wengine wanaodai anajijenga kisiasa kwa ajili ya chaguzi zijazo na wala si uchaguzi wa 2015. 

Taarifa kamili ya Makamba aliyekutana na wanahabari wa mjini Iringa hii leo, itakujia jioni ya leo

Eendelea kusubiri...............................

Reactions:

0 comments:

Post a Comment