Wednesday, 22 October 2014

JANUARI MAKAMBA AWAAHIDI BODABODA WA IRINGA KUWATAFUTIA PIKIPIKI ZA MKOPO WA MASHARTI NAFUU


Januari Makamba alipokuwa akitoa ahadi kwa bodaboda wa mjini Iringa
Hivi ndivyo msafara wa Makamba na bodaboda ulivyokuwa
Alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi na vijana
Bodaboda wakiashiria kumkubali
Kabla ya kuondoka Mwenyekiti wa Bodaboda Iringa, Mwambope Joseph akamtaka asaini kitabu cha wageni
CHAMA cha madereva wa bodaboda manispaa ya Iringa kimelamba bingo baada ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba kuwaahidi kuwatafutia kampuni itakayowakopesha pikipiki kwa bei na masharti nafuu.

Makamba alikutana na madereva hao zaidi ya 100, Jumanne ya wiki hii, baada ya kushiriki mahafali ya 13 ya kidato cha nne ya shule ya sekondari Mtera iliyopo Iringa Vijijini.

Mapokezi ya kiongozi huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), yalianzia katika eneo la Sambala mjini Iringa.

Baada ya kupokelewa, madereva hao waliokuwa wamevaa sare yao maalumu, walimuongoza hadi zilipo ofisi zao jirani na uwanja wa Mwembetogwa unaotumiwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kisiasa na kupewa ahadi hiyo.


Viongozi wa madereva hao walitarajia kusafiri jana kuelekea Dar es Salaam kufuatilia ahadi hiyo ya Makamba itakayowawezesha kupata katia ya pikipiki 50 na 100 za mkopo wenye masharti nafuu kama taratibu muhimu zitazingatiwa.

Itaendelea......................................

Reactions:

0 comments:

Post a Comment