Sunday, 19 October 2014

HALMASHAURI KUU YA CCM YAMTHIBITISHA MTENGA KUWA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA

Mtenga wa pili kulia akipiga makofi katika moja ya shughuli za chama hicho
HALMASHAURI Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemthibitisha rasmi Hassan Mtenga kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa katika kikao chake kilichofanyika hivikaribuni mjini Dodoma.

Kabla ya kukaimu kwa muda mrefu nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na aliyekuwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Mteming’ombe; Mtenga alikuwa Katibu wa CCM wa Manispaa ya Iringa. Alikuja katika manispaa hiyo akitokea wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Kabla ya kuthibitishwa katika nafasi hiyo, taarifa ya kikao hicho imeelezwa na baadhi ya wajumbe waliohudhuria kwamba; Mtenga amesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha hadhi ya CCM tangu awasili mkoani Iringa.

Taarifa ya chama hicho iliwataka viongozi wengine katika maeneo yenye upinzani mkubwa kutumia mbinu zinazotumiwa na CCM mkoa wa Iringa kufufua hali na matumaini waliyonayoa watanzania dhidi ya chama hicho.

Alipotafutwa jana kwa njia simu Mtenga alikiri uteuzi wake kuthibitishwa na akaahidi kuendeleza mapembano wakati wakielekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa madiwai, wabunge na Rais utakaofanyika mwakani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment