Saturday, 18 October 2014

FUNDI VIATU AFARAKI BAADA YA KULALA NA RAFIKI YAKE WA KIKE


Fundi radio maarufu mjini Singida, Daniel Mosha (50), amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini hapa, baada ya kuugua ghafla akiwa amelala katika nyumba ya kulala wageni na rafiki yake wa kike.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela alisema kuwa fundi huyo amefariki dunia Oktoba 14 saa 10.30 jioni katika nyumba ya kulala wageni ya Cheyo alipokuwa chumba namba nne.

Alisema Mosha alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa mjini Singida.

Alisema kuwa Oktoba 13 jioni marehemu akiwa na rafiki yake wa kike wa muda mrefu ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Manguanjuki, Manispaa ya Singida(jina tunalo) walipanga chumba katika nyumba hiyo ya wageni kwa ajili ya mapumziko ya usiku mzima.

“Ilipofika alfajiri saa 11 Oktoba mwaka huu, mwanaume huyo alianza kuugua ghafla huku akikoroma, ndipo mwalimu huyo alitoa ripoti juu ya hali mbaya ya mpenzi wake wa muda mrefu kwa meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni,” alisema na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali chumbani zilikutwa paketi tupu za pombezilizotumika.
chanzo; mwananchi.co.tz

Reactions:

0 comments:

Post a Comment