Tuesday, 28 October 2014

BULEMBO AMZAWADIA SH MILIONI MOJA MWANAFUNZI WA SEKONDARI YA MWEMBETOGWA

Diwani wa Kata ya Makorongoni, Tadeus tenga akimkabidhi zawadi, Idrisa Hamis ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdala Bulembo amemzawadia Sh Milioni moja Idrisa Hamis baada ya kuwa mmoja kati ya wanafunzi 10 waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu.

Hamis ni mmoja kati ya wanafunzi 156 waliomaliza kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Mwembetogwa ya mjini Iringa inayomilikiwa na jumuiya hiyo ya CCM.

Pamoja na Bulembo, shule ya  hiyo imemzawadia mwanafunzi huyo Sh 500,000 taslimu na kufanya jumla ya fedha alizojipatia mwanafunzi huyo kuwa Sh Milioni 1.5.


Hamis ambaye tayari amekwishajiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikabidhiwa kitita hicho katika mahafali ya 28 ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika hivikaribuni shuleni hapo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment