Friday, 24 October 2014

BAADA YA VURUGU NA KUCHOMA BWENI, KILA MWANAFUNZI NJOMBE SEKONDARI KULIPA SH150,000

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulgance Ngonyani akiangalia bweni la shule ya sekondari Njombe lililoteketea kwa moto
SHULE ya sekondari ya Njombe (Njoss) imefungwa kwa mwezi mmoja baada ya wanafunzi wake kufanya vurugu, kuchoma bweni na mali zingine za shule hiyo na kusababisha hasara inayokadiriwa kuwa sh Milioni 100.


Ili kufidia hasara hiyo, kila mwanafunzi wa shule hiyo atatakiwa kurejea shuleni hapo akiwa na mzazi au mlezi wake pamoja na Sh150,000 kwa ajili ya kufidia mali zilizoharibiwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment