Monday, 8 September 2014

WAFAHAMU VIJANA WA CCM WALIOTANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS, HUU NI WASIFU WA JANUARI MAKAMBA

Januari Makamba
VIJANA wawili ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wametangaza; wametangaza nia ya kuwania nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini. Nafasi hiyo si nyingine, mmojawapo anataka kuwa Rais.

Vijana hao ni Januari Makamba na Dk Hamis Kigwangala; Januari Makamba alizaliwa Januari 28, 1974 (ana miaka 40 hivi sasa) na Dk Kigwangala alizaliwa Agosti 7, 1975 ( ana miaka 39 hivi sasa)

Tunapenda kuwazungumzia wagombea hao hasa kwa kuwa wameshatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.

Tukianza na

JANUARI MAKAMBA
Huyu ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia. Amefanya kazi Ikulu kama mwandishi wa hotuba za Rais ndani na nje ya nchi kwa miaka mitano.

Amekuwa katika sekretarieti ya Baraza la Mawaziri kwa miaka mitano pia. Ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga aliyeaminiwa na Rais akapewa Unaibu Waziri.

Amewahi pia kuwa katibu wa Sekretarieti ya CCM Makao Makuu Idara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Ni kijana msomi na mwenye nguvu na ushawishi mkubwa kisiasa.

Alizaliwa Januari 28, 1974 (ana miaka 40 hivi sasa) na atakuwa na miaka 41 Januari mwakani.

Januari ameoa na ni baba wa watoto wawili.

Kesho BONGO LEAKS itaendelea kumchambua Januaru Makamba kabla ya kuendelea na Dk Kigwangala……………………………..

Reactions:

0 comments:

Post a Comment