Saturday, 13 September 2014

VYUO 19 VYAPATA USAJILI WA AWALI NJOMBE


MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi Kanda ya Nyanda za Juu imetoa vyeti vya usajili wa awali kwa vyuo 19 vya fani mbalimbali vya Mkoa wa Njombe.

Mtafiti wa Masoko wa Mamlaka hiyo, Susan Magani alisema vyuo hivyo vinatakiwa kufundisha fani zile zilisajiliwa na kujiendeleza ili vipande madaraja.

“Wamiliki wa vyuo hivi mnatakiwa kutoridhika na idadi ya fani mnazotoa, mnayo nafasi ya kusajili fani nyingine ili muendane na mahitaji ya jamii,” alisema wakati akikabidhi vyeti hivyo.


Naye mratibu wa mafunzo John Mwanja  aliwataka wamiliki wa vyuo hivyo kutambua tofauti ya madaraja na kufauata sheria ya kupata usajili wa kudumu katika kipindi cha miaka miwili kwani wasipofanya hivyo watalazimika kuanza hatua ya kwanza kama ilivyokuwa awali. 

Vyuo hivyo ni pamoja   na chuo  cha ufundi stadi cha  Uwemba , Ilembula Lutheran, Uvikanjo, Kipengere,I limiwaha, Profesional Collage of Njombe, Lukungu, Lugalawa, Matembwe Masimbwe Ilembura RC,MCF Makambako, Nila"s Secretarial, Makambako, Mlando Workshop, Nazareti Njombe, Igwachanya Gilgal IDT na Mpechi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment