Sunday, 7 September 2014

MAKORONGONI FC YAZOA MAHELA YA HEPAUTWA CUP

Hepautwa akikabidhi kwa kapteni wa Makorongoni FC kikombe baada ya timu hiyo kutwaa ushindi wa Hepautwa FC
Nuhu Mwasumile akimkabidhi kapteni wa Makorongoni FC kitika Sh Milioni moja baada ya kutwaa ubingwa wa Hepautwa Cup
Mashibiki 
Katika picha ya pamoja
LIGI soka ya mtoano iliyojipatia umaarufu mkubwa mjini Iringa na kushirikisha timu 16 kutoka kata zote za manispaa ya Iringa ya Hepautwa Cup imehitimishwa jana kwa timu Makorongoni FC kutwaa kombe na Sh Milioni moja taslimu baada ya kuichabanga bila huruma Kitanzini kwa FC kwa mabao 3-0.

Kipindi cha kwanza cha mtanange huo uliopigwa katika uwanja wa Samora mjini hapa,kilimalizika kwa timu hizo zenye mashabiki lukuki kutoona nyavu ya mwenzake.

Magoli yote matatu ya Makorongoni FC yalifungwa kipindi cha pili cha mchezo huo uliokuwa na kasi ya ajabu kutoka kwa timu zote mbili.

Ilikuwa katika dakika ya 66, kiungo wa kati wa Makorongoni FC, Leonard Geka alipopokea pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji mwenye uchu wa magoli na kipaji cha pekee David Mhanga (17) na kuwahada walinzi wa Kitanzini FC kabla hajapiga shuti kali lililomshinda golikipa wa Kitanzani FC.

Magoli mawili yaliyoihakikishia ushindi Makorongoni FC yaliwekwa kimiani na David Mhanga aliyeibuka mchezaji bora wa ligi hiyo katika dakika 86 na 90.

Mbali na Makorongoni FC kujinyakulia zawadi hizo, Kitanzini FC waliondoka na Sh 600,000 taslimu huku Kihesa FC ikijinyakulia Sh 300,000 baada ya kupata ushindi wa chee kufuatia timu ya Mshindo FC kuingi mitini.

Zawadi hizo zilikabidhiwa kwa timu hizo na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Iringa, Nuhu Mwasumile.

Mdhamini wa mashindano hayo Nuru Hepautwa alisema amefurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na wachezaji wa timu zote zilizoshiriki ligi hiyo na akahidi kuongeza zawadi kwa washindi na timu shiriki mwakani.

Aliwataka wachezaji hao kuendelea kufanya mazoezi na kujituma katika mashindano watakayokuwa wanashiriki kwani michezo inaweza kuwa ajira nzuri kwao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment