Sunday, 14 September 2014

MAHAMUDU MADENGE AZIMWAGIA TIMU ZA SOKA ZA IRINGA VIFAA VYA MICHEZO

MNEC Mahamudu Madenge (mwenye suti) akikiabidhi vifaa kwa timu ya Mlandege


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mahamudu Madenge ameahidi kushirikiana na wadau wa michezo wa mjini Iringa kuiboresha sekta hiyo.

Aliyasema hayo hivikaribuni alipotoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za Lipuli, Mlandege na Mshindo.

Madenge alisema; “hii ni kiu ya kila mmoja, tunataka kuona Iringa inakuwa na timu inayoshiriki ligi kuu, lakini hatuwezi kufika huko kama hatutakuwa na mipango ya kukuza mchezo huo kuanzia ngazi ya chini kabisa.”

Alisema katika kipindi chake chote atakachokuwa mjumbe wa NEC atahakikisha timu zenye lengo la kufika mbali zinasaidiwa.

“Nawakaribisha na wadau wengine, wasaidie timu zetu hizi, kwa kufanya hivyo zitajiona ziko pamoja na wananchi wao na hivyo kuongeza juhudi katika mchezo huo,” alisema wakati akizikabidhi timu hizo jezi na mipira.


Alisema katika kuongeza hamasa, ataiomba timu ya ligi kuu inayosaidiwa na kiwanda chake cha maji ya Ndanda, Ndanda FC ya Mtwara ifanye ziara mjini hapa ili ipate fursa ya kucheza na timu yoyote itakayokuwa tayari.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment