Monday, 8 September 2014

KIJANA APIGWA HADI KIFO AKITUHUMIWA KWA USHIRIKINA

Marehemu Mwasyebule enzi za uhai wake
MATUKIO ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi ya maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio la jana  kijana  wa miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alimtaja aliyeuawa katika tukio hilo kuwa ni Gabriel Mwandemwa (maarufu kwa jina la Mwasyebule).

Mwasyebule ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ikamambande Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kifuani.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana majira ya saa tano asubuhi katika Kijiji hicho kilichopo kata ya Lwangwa, Tarafa ya Busokelo wilayani Rungwe.

Taarifa za awali zinadaiwa kuwa uongozi wa kimila kijijini hapo  uliitisha kikao cha dharura kilichohusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani.

Kabla ya kikao hicho iliamuliwa Mwasyebule atufutwe popote alipo ili awe kuhudhuria kikao hicho.

Katika kikao hicho marehemu alituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ushirikina kijijini hapo kwa kuwaroga watoto na kuwatumikishi kishirikina watu mbalimbali katika mashamba yake ili ajipatie mazao mengi.

Taarifa hiyo iliwapa jazba baadhi yao na kuamua kumpiga hadi kifo chake.

Na Mbeya yetu Blog


Reactions:

0 comments:

Post a Comment