Thursday, 4 September 2014

HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA YAKAMILISHA UJENZI WA MAABARA SEKONDARI YA ISIMANI NA NYANG'ORO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka
HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa imetangaza kukamilisha ujenzi wa maabara za sayansi, bweni la wasichana na chumba cha darasa katika shule za sekondari Ismani, Nyang’oro na Kalenga.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Pudenciana Kisaka  alisema wakati maabara iliyojengwa katika shule ya sekondari Ismani kwa zaidi ya Sh Milioni 89 inatumika kwa masomo ya Bailojia:

Katika shule ya sekondari Kalenga jumla ya Sh Milioni 29 zimetumika kujenga maabara mbili za masomo ya Fizikia na Kemia huku Sh Milioni 258 zikitumika kujenga bweni la wasichana.

Kisaka alisema katika shule ya sekondari Nyang’oro wamejenga chumba kimoja cha darasa kilichogharimu sh. Milioni 13.

Akizungumzia mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu, alisema halmashauri hiyo itapokea jumla ya wanafunzi 2,389 tofauti na wanafunzi 1,433 iliyopokea mwaka katika shulezake sita zinazotoa elimu hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment