Saturday, 13 September 2014

AKAMATWA MAKORONGONI MJINI IRINGA NA DAWA ZA KULEVYA


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Pudenciana Protasa amesema jeshi la Polisi limemkamata na kumtia nguvuni Allein Aldo baada ya kukutwa na kete 19 za dawa za kulevyam aina ya Cocaine.

Alisema Aldo alikamatwa Septemba 11, majira ya saa 5.30 asubuhi wakati askari polisi wakiendelea na doria yao ya kawaida katika maeneo ya barabara mbili, mjini Iringa.

Alisema mtuhumiwa alikutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya akiwa ameficha kwenye mfuko wa suruali aliyovaa katika harakati zake za kuwapelekea wateja wake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment